Usilipe pesa yoyote kabla ya kuona mali na kuthibitisha umiliki.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Majibu ya maswali yanayoulizwa mara nyingi kuhusu kupanga, kununua na usalama.

BnB

Naweza kughairi booking ya BnB?

Ndiyo, kulingana na sera ya mwenyeji (Flexible, Moderate au Strict) iliyoandikwa kwenye tangazo.

Jumla

Property ID ni nini?

Ni namba ya kipekee ya kila tangazo, kwa mfano KNS-DSM-UBU-000002. Itaje kwenye simu au WhatsApp ili tujue unaongelea mali gani.

Kuweka tangazo ni bure?

Ndiyo, kila mwenye mali anaweza kuweka matangazo kadhaa bure. Mawakala na kampuni wana vifurushi vyenye matangazo zaidi na matangazo maalum.

Video ya tangazo inaweza kuwa ndefu kiasi gani?

Hadi dakika 3 (au kiwango kilichowekwa na msimamizi). Unaweza pia kuweka link ya YouTube au TikTok.

Malipo

Ninalipaje?

Kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au kadi. Kwa sasa unalipa kwa Lipa Namba kisha unaweka namba ya muamala; tunathibitisha ndani ya muda mfupi.

Kupanga

Kodi ya mbele ni miezi mingapi?

Inategemea mwenye nyumba (kawaida miezi 3, 6 au 12). Kila tangazo linaonyesha idadi na jumla utakayohitaji.

Kununua

Nifanye nini kabla ya kununua kiwanja?

Kagua hati, fanya official search Ofisi ya Ardhi, tumia wakili kwa mkataba, na usilipe pesa nyingi kabla ya uhakiki.

Usalama

Beji ya "Imethibitishwa" inamaanisha nini?

Kuna ngazi 4: simu, kitambulisho (NIDA), hati za umiliki, na ukaguzi wa eneo. Bonyeza beji kuona kiwango.

Hujapata jibu? Tuko hapa kukusaidia.
Wasiliana nasi
Tuandikie